WASTARA Aandika Ujumbe Wakusikitisha Kuhusu Maisha yake ‘Nahisi Mauti Yapo Karibu Yangu’ - MULO ENTERTAINER

Latest

2 Jan 2017

WASTARA Aandika Ujumbe Wakusikitisha Kuhusu Maisha yake ‘Nahisi Mauti Yapo Karibu Yangu’

Msanii wa filamu Wastara Juma ameandika barua ya wazi kueleza jinsi anavyojisikia ikiwa ni miaka 5 toka ampoteze mume wake marehemu Sajuki Juma.


Muigizaji huyo amedai toka ampoteze mume wake huyo hajawahi kupata furaha katika maisha yake licha ya kujaribu kufanya kila awezavyo.

Yakiwa yamebaki masaa machache kabla ya mwaka 2016 kumalizika, mrembo huyo kupitia facebook ameanda ujumbe huu.

Naanza kwa kumshukuru mungu wangu anaenipa pumzi ya bule mpaka mda huu, Sina budi kusema haya nitakayoyasema kwa ajili mwaka mpya unaonza kesho. Ni miaka 5 na miezi 6 leo imetimia toka furaha yangu ilipoingia dosari .

Mungu alinipa mtu wa kunipa furaha kwasababu kilakitu Alhamdulilah nilikuwanacho kulingana na nafasi yangu lakini sikuwa na furaha lakini furaha hiyo haikudumu nakumbuka ilikuwa mwezi 6/ 2011 marehemu Sajuki alipoanza kuumwa ndipo furaha ilipoanza kupotea kwa sababu sikupata nafuu wala moyo wangu kupumzika mpaka leo tarehe 31/12/2016 nimejaribu kutafuta furaha kila sehemu kila njia ila imeshindikana, kuishi katika mazingira hayo kwa mtu mwengine angekuwa kama kizee hata kuchana nywele ingekuwa shida ila katika maisha ya maumivu na Sajuki siku moja aliniambia mke wangu mi naumwa ila sipendi kukuona ukiwa mchafu na pia usinizuie kwenda kokote sababu nitakufa siku yoyote tutumie muda uliobakia kufanya kile kitu moyo unataka.

Nami kwasasa naishi hivyo nahisi mauti yapo karibu yangu sana hivyo kile moyo wangu unataka ndicho nakifanya hata moyo ukiniambia inuka na maumivu yako nipeleke baharini basi naupeleka uko ukisema nipeleke disco naupeleka uko ukisema nikakeshe msikitin naupeleka uko hivyo sitabariki na sipendi kuishi ili mtu anione nina maumivu nalazimisha furaha japo aipo hivyo mnisamehe wale wote msionielewa kokote mkinikuta mniche tu sifanyi kitu kumkera mtu i need peace of mind,moyo wangu maskin unanivuja damu kilasiku natamani nifanye lolote ili upumue hakuna kitu kibaya kama kupoteza furaha na tumain unaishi kama uko dunia ya peke yako nimeongea haya ili muelewe hisia zangu kuwa hata ukiongea kitu ambacho sijakifanya sihusiki au kunitafsiri vibaya naumia mara 2 nahisi kama na wew ni mmoja ya wale wasiopoenda kuona nikifurahia uwepo wangu duniani.

Viongozi wangu ndugu jamaa wasanii wenzengu na mshabiki wangu nawaomba kwa pamoja mpige goti kuniombea 2017 moyo wangu upate furaha ya kudumu upate dawa ya maumivu upate tabasamu la kweli na sio feki ninalotoa sasa aniondoshee maradhi yote
moyo wangu unahitaji furaha masikin mwaka 2017 uwe na neema kwetu sote ameen