‘Mnamuonea Wema Sepetu’, Mashabiki Wake Nchini Kenya Walalama - MULO ENTERTAINER

Latest

7 Feb 2017

‘Mnamuonea Wema Sepetu’, Mashabiki Wake Nchini Kenya Walalama


Wema Sepetu ni miongoni mwa mastaa wakubwa wa Tanzania walioitwa na kufika katika kituo cha polisi cha central jijini Dar es Salaam ili kujibu tuhuma za kuhusishwa na dawa za kulevya.

Habari hizi ambazo zimesambaa kwa nguvu kama vile moto kwenye mbuga ya wanyama wakati wa kiangazi na kuzagaa kwenye vyombo mbambali vya habari Afrika Mashariki, zimewashutua wengi haswa mashabiki wa malkia huyo wa filamu Afrika.

Si ndani ya nchi ya Tanzania pekee ambapo mashabiki wa Wema Sepetu wameteta kuhusu staa huyo kudhalilishwa kwa kuhusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya bali hadi hapa ndani ya nchi ya Kenya.

Naziangazia baadhi ya nukuu za waziri Nape ambazo zimeonyesha kuwa waziri huyo hakufurahishwa wala haungi mkono jinsi zoezi hilo lilivyofanyika, “Lazima itumike busara, tusiwahukumu watu kwa tuhuma, kutengeneza brand ni kazi kubwa sana wakati kuibomoa ni jambo la sekunde tu. Kama wizara tunaunga mkono juhudi za kupambana na dawa za kulevya, tatizo ni namna ya kushughulika na wahusika ikiwemo busara. Tunaunga jitihada za mapambano lakini ni vizuri lifanywe katika namna ya kulinda haki ya mtuhumiwa ili heshima yake isipotee.”

Huu ulikuwa ukweli mtupu kutoka kwa waziri Nape, maana alijua athari za kuwatuhumu wahusika hasa ikizingatiwa baadhi yao ni watu mashuhuri nchini Tanzania.

Athari hizo zimeaanza kuonekana si Tanzania pekee bali Afrika Mashariki labda na bara zima la afrika. Kwenye mitandao ya kijamii, vituo vya redio na hata runinga Afrika Mashariki, habari hizo zimetengeza headlines zenye uzito.

Katika mchakato huo, tovuti moja maarufu nchini Kenya kwa jina, ”Nairobi News” kama vyombo vingine vya habari nchini Kenya liliitumia fursa yake kuwasilisha kwa mashabiki wake habari hizi kwa kichwa kilichosem, ‘Top Tanzanian celebrities linked to drug trafficking’ nakushare habari hii kwenye Fan-page yao ya Facebook.

Wengi walio tupia comments zao, walionekana kuegemea kukashfu vikali kutajwa kwa jina la Wema Sepetu kwenye kashfa hiyo. Hii ni ishara ya kuwa Wema Sepetu anakubalika na kupendwa na halaiki ya mashabiki hapa nchini Kenya, na nikiwakumbusha tu, kuna wakati mwaka jana 2016 Sepetu alizulu Kenya na akakaribishwa vizuri hadi akaeleza kupitia mtandao wa kijamii jinsi alivyo karibishwa Kenya na huenda akafikiria kuhamia nchini humu.

Hizi hapa chini ni baadhi ya comments za wakenya na headline kutoka kwa ukurasa wa Facebook wa tovuti ya Nairobi News.

Maggie Nyawi

mmmh……..when will u stop interfering with others pples international
affairs?……if it’s true or into what will ugain
by gossiping n telling public?

Annitah Walcoltt

Wema ain’t this crap…..Spare my Wema

Omar Elmy

its not true

Sharon Phiny
Even Wema Sepetu and Idriss have been mentioned and they look innocent?


Makala ya: Changez Ndzai