Vita dhidi ya Dawa za Kulevya: Iddi Azzan, Hussein Pamba Kali na Bosi wa Sea Cliff Watua Central Polisi - MULO ENTERTAINER

Latest

11 Feb 2017

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya: Iddi Azzan, Hussein Pamba Kali na Bosi wa Sea Cliff Watua Central Polisi

Aliyekuwa mbunge wa Kinondoni Iddi Azzan, bosi wa Sea Cliff pamoja na watuhumiwa wengine wa sakata la biashara ya Madawa ya kulevya wamefika polisi kituo cha kati kutii wito wa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

Watuhumiwa 65 wa biashara ya Madawa ya kulevya katika list ya pili ya Mkuu huyo wa mkoa wa Dar es salaam Walitakiwa kuripoti central polisi Ijumaa hii.

Hata hivyo kati ya watuhumiwa hao, Manji pamoja na Askofu Gwajima waliripoti kituoni hapo jana na taarifa ambazo zilizagaa mitandaoni walipelekwa kwa mkemia mkuu kupimwa.