Mzee wa Upako Kashusha Nyundo Hizi Baada ya Gwajima Kutajwa Sakata la ‘Unga’...!!! - MULO ENTERTAINER

Latest

11 Feb 2017

Mzee wa Upako Kashusha Nyundo Hizi Baada ya Gwajima Kutajwa Sakata la ‘Unga’...!!!

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ ameshauri kuwapo kwa utaratibu maalumu wakati wa kuwaita kwa mahojiano watu wanaoitwa kwa mahojiano kuhusu dawa za kulevya.

Mzee wa Upako alisema hakukuwa na umuhimu wa vyombo vya habari kuhusika katika kuwataja watu hao hasa viongozi wa dini, bali wangeitwa kwa barua maalumu. Alisema inapotokea wachungaji wakahusishwa na dawa za kulevya ni muhimu kuwapo na ushahidi wa kutosha kinyume na hapo, itawavunjia heshima yao.

Mzee wa Upako alisema anaunga mkono kwa asilimia zote vita dhidi ya dawa za kulevya ila hajafurahishwa na namna suala hilo linavyofanyiwa kazi hali inayoweza kuwaharibia watu heshima.