BAADA ya mkewe, Nawal kujifungua mtoto wa kike, Mwanamuziki wa Bongo
Fleva, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ ameamua kumzawadia wimbo ikiwa ni
njia ya kumshukuru kwa kuwa ni mwanamke wa kipekee kwake kuliko aliowahi
kutoka nao kabla hajaingia kwenye ndoa.
Akichezesha taya na Mikito Nusunusu, Nuh alisema anajivunia kupata mtoto
wa kike aliyempa jina la Anyagile japokuwa alitamani angepata wa kiume
lakini hana budi kumpokea kwa furaha ndiyo maana ameamua kumzawadia
mkewe wimbo unaokwenda kwa jina la Anameremeta.
“Namshukuru Mungu kwa kunipa mtoto Jumatatu iliyopita, siku iliyofuata
nikatoa wimbo huo ambao ni zawadi kwa mke wangu kwani ni mwanamke wa
tofauti kwangu kwani kanizalia mtoto mzuri ambaye ndiye wa kwanza
kwangu, nina furaha sana kwa kweli,” alisema Nuh Mziwanda.