Jinsi Ya Kuingia Katika Akili Ya Mwanamke..!!!
Je uko tayari kufahamu jinsi ya kuingia katika akili ya mwanamke na
kufanya mapinduzi ya njia ya kawaida unayotumia kuapproach mwanamke?
Kama jawabu lako ni ndio, basi zama nami kusoma hizi mbinu ambazo
zimethibitishwa kufanya kazi.
1. Anza approach ya mbali
Kabla ya kumuapproach mwanamke, hakikisha ya kuwa unamsoma kwa umbali
mambo anayofanya kwanza. Halafu ukiona kama umepata kile unachoweza
kutumia kutoka kwake unaweza kumuaproach. Ukiwa unaongea nayeye mwambie
kuwa una uwezo wa kusoma nyota yake.
Wanawake wengi watakubaliana na hili ili kuona ucheshi wako. Halafu
ukirudilia na vitu ambavyo ulimsoma awali, utakuwa umemfunga. Mwanzo
kama umejaribu kumtabiria vitu ambavyo viko sawa kwake ama vinahusiana
na yeye, una nafasi kuu ya kumfanya kukutaka kukufahamu zaidi. Pia ni
vizuri kufahamu miondoko ya wanawake na mapema ili kuelewa kama
anakubaliana na utabiri wako kwake.
Pia unaweza kuwambia unaweza kusoma nyota yake kupitia kwa maganja yake.
Hii itakupa nafasi ya rahisi kuweza kupata kumgusa bila kukushuku
ajenda yako nzima iliyo akilini mwako. Mbinu hii itamfanya yeye kuvutiwa
na wewe kwa urahisi.
2. Leta shangwe
Wanawake wanapenda wanaume ambao hawayachukulii maisha serious vile, so
hakikisha kuwa unajua jinsi ya kuchat na wanawake. Unaweza kutumia
mbinu ya kutumia kuwa mcheshi na kutoa mizaha ukiwa kando yake. Kufanya
hivi kutamfanya yeye kucheka na kutabasamu, jambo ambalo automatic
litamfanya yeye kuvutiwa na wewe. Usitumie mbinu ya kumtesa sana na
mizaha yako ama utaonekana kuwa na utoto mwingi ama anaweza
kukasirishwa. Uzuri wa kutumia ucheshi ni kuwa kunamfanya mwanamke
kujihisi bado ana ujana.
3. Ichokore akili yake
Hii ni mbinu ya sanaa ya kutongoza ambayo itamfanya mwanamke yeyote
kuathirika kihisia na wewe. Itamfanya akutamani na kuifanya akili
kukufikiria wewe tu.
Njia moja kama hii ni kumfanya mwanamke kuingiwa na furaha dakika moja
na kukasirika dakika ya pili. Wanawake inaonekana mara nyingi hupenda
vioja katika maisha yao, kama vile katika vipindi vya tamthilia ama soap
opera. Hoja ya vioja ni nzuri pia kwa kuwa inatoa ile dhana ya
kubandikwa jina kuwa unaboa.
Kama unaweza kuyafanya maisha yako kuwa na vioja vya mara kwa mara
wanawake watakupenda automatically bila wao kujifahamu. Ukishafanikiwa
kuteka hisia zao, inakuwa rahisi kwako kuingia katika akili yao. Unafaa
kuonywa ya kuwa kutumia mbinu hii sana inaweza kuwafanya baadhi ya
wanawake kuchunguza maisha yako wakitaka kuwa karibu yako kila wakati.
Pia fahamu ya kuwa usimchangaye akili kihisia mwanamke yeyote kwa kutumia mbinu hii kwani mwishowe inaweza kukujeukia.