Samatta Azifuata Mwenyewe Arsenal na Chelsea - MULO ENTERTAINER

Latest

28 May 2018

Samatta Azifuata Mwenyewe Arsenal na Chelsea

Samatta azifuata mwenyewe Arsenal na Chelsea
Bao la kwake mwenyewe pamoja na jingine la Jere Uronen, yamemwezesha mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta kuzifuata klabu za Arsenal na Chelsea kwenye Kombe la Europa msimu ujao.


Samatta alifunga bao la kwanza kwenye mchezo wa ligi kuu ya Ubeligji usiku wa jana na kuisaidia timu yake KRC Genk kupata tiketi ya kucheza michuano ya Europa League baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Zulte Waregem.

Samatta alifunga bao hilo dakika ya 18, huku mlinzi Jere Uronen akifunga la pili dakika ya 28 akimalizia kazi nzuri ya kiungo Alejandro Pozuelo Melero. Genk watalazimika kuanzia raundi ya 3 ili kufuzu kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Mechi za raundi ya 3 zitachezwa kati ya Agosti 9 na 16 mwaka huu na endapo Genk itafuzu hatua hiyo, itaungana na timu za Arsenal na Chelsea kutoka England katika hatua ya makundi ya michuano hiyo itakayoanza Septemba 20.

Samatta sasa amefikisha mabao 26 katika mechi yake ya 90 tangu ajiunge na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).