Ally Kiba Awachanganya Mashabiki Wake - MULO ENTERTAINER

Latest

16 Aug 2017

Ally Kiba Awachanganya Mashabiki Wake

Ally Kiba Awachanganya Mashabiki Wake
Mkali wa sauti na mwenye 'hit song' ya 'Aje', Alikiba amewaacha njia panda watu wake wa karibu pamoja na mashabiki wa kazi zake baada ya yeye kuweka picha katika mtandao wake wa Instagram ukiwa na neno 'wananiita Kipusa'

Muda mchache kupita mashabiki hao walimiminika katika picha hiyo kwa kutoa maoni yao binafsi, huku wengine wakijaribu kubashiri kuwa  huenda ni ujio wake mpya wa nyimbo anayotarajiwa kuiachia katika siku za hivi karibuni.

Miongoni mwa ujumbe zilizokuwa zikitawala chini ya tangazo hilo ni pamoja na;
Rajo Jr: Alikiba bana, katisha na atapita hivi hivi na kutuacha na mihamu yetu hahaha. King ni 'undefined musician' unaweza kuta kipusa siyo nyimbo ila kauliza tu kuwa wanamuita kipusa?, kwa sababu tuna hamu ya kumsikia tumewaza ngoma mpya.

Careen Candy: Nafuu leo imekua siku nzuri maana ulishaanza kuniboa hata wanangu wakikuona kwenye runinga walikuwa wakiniita lakini sikuweza kutoka ndani.

Official george :siye tunataka ngoma, hatutaki maneno maana tumechoka kunyanyasika huku mtaani.

Costz himself: Tunavyoijua 'Team' Fulani muda huu watakuwa wanapanga kuishambulia kipusa, na wahakikishieni Kipusa ikitoka basi na wao wote wataachia ngonjela zao zinazopigwaga shuleni akija mgeni.

Inno_Kalinga: Waachie washindane na jina la nyimbo kwa wiki mbili kwanza.

Karim Issa: Mungu akusimamie unstoppable utuletee ngoma Kali, maana tumechoshwa na mavuvuzela.

Babesh Sultan: sawa si kwa kutususa hivi king, wengine washapata matatizo ya moyo kusubili ngoma. Iachie mzee baba kitaani hatuna raha kabisa.


Kwa upande mwingine, hayo yote yametokana na ukimya wa kipindi kirefu cha Alikiba jambo ambalo limepelekea mashabiki zake kuanza kufurahia jambo ambalo hata hawalifahamu kiundani kwamba Kipusa ni ujio wa nyimbo yake mpya au pengine msanii huyo ameamua kubadilisha jina na kujiita hivyo au pengine ameamua kuja na 'product' zake ambazo zitakuwa zikiitwa kwa jina hilo.

Alikiba siku ya Jumamosi anatarajia kufanya show katika mji wa New York, Marekani ambapo atakuwa na wasanii wengine kama P Square, 2 Face Idibia, Tiwa Savage  pamoja na Cassper Nyovest.