Duniani Kwa Sasa ina Marais Watano tu...Magufuli Akiwa Mmoja Wapo.... - MULO ENTERTAINER

Latest

7 Aug 2017

Duniani Kwa Sasa ina Marais Watano tu...Magufuli Akiwa Mmoja Wapo....


Kwa maoni yangu na kwa kuangalia kwa makini kulingana na mahitaji ya kidunia kwa sasa kuna wanaume watano tu ndio wanaweza kusimama wakaongea na mimi nikaelewa kuwa hawa in maraisi ingawa wote wana mapungufu yanayofanana juu ya Democracy.....
Magufuli :
Rais anayepigania masilahi ya watanzania kwanza na wazungu baadae..
Kafanikiwa kuwabana wazungu walipe Kodi kama alivyofanya kwa acacia.

Kama alivyofanya kwa wafanyabisha wengine kukimbia bandari ya Dar kisa tu sheria ya kodi iliyokuwepo toka enzi za kikwete ilianza kusimamiwa kwa umakini...

Kilichonivutia zaidi ni idadi ya miradi aliyoizindua ndani ya miaka miwili kama fly over DSM, Ujenzi wa Reli ya dar morogoro,miladi ya kiisitoria ya maji tabora, Sengerema ambako watu wako karibu na ziwa kilometer 3 walikuwa hawana maji miaka 55 ya Uhuru?...,na mwisho mradi wa bomba la mafuta kwenda Uganda hili ndio historia bora kabisa likikamilika...

Jambo lililonifuraisha zaidi mwaka huu wa fedha tupo na Ajira 52000 kiukweli kama tutashindwa kumsapoti Rais kwenye mambo muhimu ya kitaifa kama haya basi inabidi tupimwe mkojo.

Rais anayepambana na wahujumu uchumi bila kumungunya maneno,nimependa falsafa yake kiufupi ni Rais ambaye Huwezi kumlingania na Rais yeyote Africa kwa sasa nisijue kama atachoka lakini kazi anayofanya zile muhimu'

Kwana nikiri kuwa mimi ni msomaji mzuri wa magazeti ya ulaya kama Daily mail,The guardian, na the Sun....

BBC, CNN na Majarida pia ya marekani hayawezi kupitisha week bila kumuongelea Rais Magufuli kwenye habari zao..

Magazeti pia ya Kenya ,Nigeria,and south Africa hawa jamaa kila week lazima waandike tukio la rais Magufuli'..

Level za Magufuli kwa sasa ni watu kama
Vladimir Putin


Rais wa urusi ambaye aliikua urusi ikiwa na hali mbaya kiuchumi na kuipaisha na kuwa super power in the world..

Naweza pia kumlinganisha Magufuli na Rais wa Marekani.

Donald Trump
Ambabaye hana mzaha na masilahi ya wananchi marekani ...
Ambaye mwezi July pekee katengeneza ajira 270,000 wakati mwaka wake wa fedha unaanza.

Mwingine ambaye naweza kumlinganisha na Rais magufuli ni Rais wa North Korea bwana

Kim-Jong-Un

Ambaye pia hataki mzaha na masilahi ya watu was north Korea....

Rais wa mwisho duniani ambaye naweza kumkinganisha na Rais magufuli ni Rais Wa Philippines

Rodrigo Duterte 

Ambaye naye hataki kabisa wauza madawa ya kulevya kama alivyo rais wetu.

Marais waliobaki wengi ni very weak na hawaendani na wakati wa dunia inataka nini kwa sasa....

Kuna muda uwa namkosoa rais wetu lakini kwenye swala la kusimamia masilahi ya taifa nipo naye bega kwa bega Rais wetu ni Rais bora kabisa duniani kwa sasa narudia tena hakuna Rais wa africa anayeogopwa na kufatiliwa na watu wengi duniani kama alivyo Rais Magufuli'

Tumuunge mkomo Rais tujenge Tanzania vyama vipo vitaendelea kuwepo sioni ubaya wa sisi kuweka itikadi pembeni na kumsaport kwenye mambo muhimu ya kitaifa kama haya anayoyafanya Rais wetu Ccm, Chadema,Cuf vitapita lakini Tanzania itabaki.


Jamii Forums/technically