Kesho ni siku ya Uchaguzi Mkuu nchini Kenya na viashiria vinaonesha kama
ilivyokawaida kwa Tawala za Kiafriak,Rais aliyeko Madarakani kwa sasa
Uhuru Jomo Kenyata huenda akashinda kwa kishindo dhidi ya mpinzani wake
Raila Omolo Odinga.
Kama ndivo itakavokuwa basi huenda matokeo hayo ya kaanzisha mnyukano
mwingine mpya kabisa ndani ya Afrika Masharaiki. Nitaeleza. Kampeni za
uchaguzi zimehitimishwa juzi Ijumaa kule jijini Nairobi huku Edward
Ngoyayi Lowassa akimpigia kampeni za nguvu Uhuru Jomo Kenyata mgombea wa
tiketi ya JUBILEE. Edward Ngoyayi Lowassa ni PM mstaafu wa Tanzania na
ndiye aliyekuwa mgombea wa Urais Tanzania mwaka 2015 kwa tiketi ya
CHADEMA under UKAWA na kuwa mshindi wa 2 kwa JPM akizoa takribani kura
miilioni 6 na ushei.
Raila Omolo Odinga mgombea Urais kwa tiketi ya NASA ni rafiki kipenzi wa
Rais wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli. Hapa ndipo kwenye kiini cha
sintofahamu baada ya matokeo ya Uchaguzi nchini Kenya hapo 8/8/2017.
Ikumbukwe kwamba Raila Omolo Odinga anachuana vikali na Uhuru Kenyata wa
JUBILEE. Raila ni PM mstaafu nchini Kenya wakti wa awamu ya Mwai
Kibaki. Je, nini kitatokea katika uhusuano wa Kenya na Tanzania kama
Uhuru Kenyata atashinda ambaye anasaidiwa wenya kampeni na Edward
Lowassa mpinzani wa Magufuli? Yamkini mambo yatakuwa supa iwapo Raila
Jaramogi Oginga Odinga atashinda ambaye ni rafiki kipenzi wa John Pombe
Magufuli. Tusubiri hatima ya mchuano huu kwani bado masaa machache tu
kuingia siku ya 8/8 ifikapo usiku wa manane. Mungu ibariki Kenya, Mungu
ibariki Tanzania na Mungu ibariki Afrika na watu wake.Amina.
7 Aug 2017
New