Aliko Dangote ana utajiri wa dola za Marekani bilioni 12.2 (trilioni 27), ambaye utajiri wake ni takriban asilimia 3 ya pato la Taifa la Naijeria, unamfanya awe mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa urahisi — na ndio bilionea mweusi aliye juu zaidi kwenye orodha ya watu matajiri duniani.
Hii ni taarifa nzuri, lakini hii ni nusu tu ya utajiri aliokuwa nao Dangote mwaka 2014 ambapo hadi mwaka huo ulipoisha, Dangote alikuwa na utajiri wa dola za Marekani bilioni 25 (trilioni 56).
Sehemu kubwa ya utajiri wake (asilimia 90) inatoka kwenye viwanda vyake vya kutengeneza saruji (Dangote Cement), kampuni iliyoorodheshwa kwenye Soko la Hisa nchini Naijeria yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 11, sawa na trilioni 24.
Biashara za bilionea Dangote zimesambaa kwenye nchi kadhaa barani Afrika. Anamiliki viwanda vya kutengeneza saruji nchini Zambia, Senegal, Tanzania, na Afrika Kusini.
Dangote, ambaye amekuwa Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa kundi la kampuni za Dangote kwa zaidi ya miaka 35 sasa pia ni mtu anayetoa misaada ya kibinadamu. Akiwa ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Misaadaya ya Dangote, anasimamia misaada katika elimu, kilimo na afya ikiwamo msaada wa dola za Marekani 12,000 (takriban shilingi nilioni 27) kwa siku kwa watu wanaokosa huduma muhimu.
“Aliko ni tajiri namba moja barani Afrika, na biashara zake zinachangia kukuza uchumi wa bara zima. Hilo ni jambo zuri, lakini namtambua zaidi kama kiongozi ambaye yupo mstari wa mbele kupunguza tofauti kati ya biashara za watu binafsi na sekta ya afya ya jamii nzima,” aliandika bilionea namba moja duniani, Bill Gates. Bilionea huyo kwenye sekta ya teknolojia almemsifu Dangote kwa mafanikio makubwa aliyochangia kuitoa Naijeria kutoka kwenye orodha ya dunia ya nchi zenye magonjwa ya milipuko kwa juhudi zake za kupambana kutokomeza ugonjwa wa polio.
Mwezi Januari 2016, Dangote na Bill Gates walitoa ahadi ya kutoa dola milioni 100 ili kutokomeza utapiamlo nchini Naijeria, nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika.
17 Aug 2017
New
Maskini..Utajiri wa Bilione Dangote Waporomoka zaidi ya Nusu...
mulo
Newer Article
Kimenuka...Aliyeisaliti CCM Kwenye Uchaguzi Kujadiliwa na Kamati ya Maadili
Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Musoma Mjini inatarajiwa kukutana na kujadili hatua ya Diwani wa Kata ya Sunguti, Denis Ekwabi kukisaliti chama hicho na kumpigia kura mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakati wa uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti uliofanyika katika Halmashauri ya Musoma Vijijini.“Sisi baada ya uchaguzi kuisha tuliitana wanachama wote wa CCM ili kutaka kujua nani aliyetusaliti wakati kwenye vikao vyetu vya ndani ya chama tulikuwa tumeshampitisha mgombea wetu atakayegombea nafasi hiyo na tukakubaliana, lakini tulipokutana tu Diwani wa Kata ya Sunguti, Denis Ekwabi alikiri mwenyewe kuwa ndiye aliyepigia kura CHADEMA,” alieleza Bernard Ghati, Katibu wa CCM Wilaya ya Musoma MjiniKatibu huyo alilaani kitendo cha Diwani huyo kukisaliti chama na kupigia kura chama kingine, akieleza kuwa ni utovu wa nidhamu na kutozingatia kanuni za chama hicho, hivyo watakapokutana na Kamati ya Maadili watatoa tamko juu ya tukio hilo.Ghati alisema kuwa idadi ya Madiwani wa Halmashauri hiyo ni 26 na Madiwani wa CCM wapo 22 na wa CHADEMA wanne, lakini kura zilipopigwa zilionesha kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti kupitia CHADEMA alipata kura tano na wa CCM alipata kura 21, kitendo kilichowafanya wanaCCM kubaini kuwa kuna mmoja wao aliyewasaliti.
Older Article
Rapa Roma Mkatoliki Aanza Kuunyemelea Ulaji wa Ubunge 2020
Polisi Tanzania kuajiri askari wapya 3,000Aug 13, 2021
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania May 23 May 23, 2019
Labels:
Habari