RC Makonda Atangaza Kihama kwa Watumishi wa Serikali Jumaosi - MULO ENTERTAINER

Latest

16 Aug 2017

RC Makonda Atangaza Kihama kwa Watumishi wa Serikali Jumaosi

RC Makonda Atangaza Kihama kwa Watumishi wa Serikali Jumaosi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda Jumamosi hii ataendesha kongamano katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) Posta kujadili hali za barabara za jiji la Dar es salaam ambapo wananchi watapewa fursa za kueleza hali za barabara kutoka mitaani kwao.

RC Makonda akisalimiana mmoja kati ya wawakilishi wa JICA, Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan, lililojenga barabara ya Samora Avenue pamoja na Bustani ya Kaburi Moja.

Makonda amesema hayo wakati akikabidhiwa barabara ya Samora Avenue pamoja na bustani ya ‘Kaburi Moja’ iliyopo katikati ya Posta Dar es salaam iliyokarabatiwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan, JICA.

Alisema Kongomano hilo litawakutanisha wadau mbalimbali wa barabara wakiwemo Tanroad, wakandarasi pamoja na wananchi kutoka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

“Jumamosi hii tutakutana na wadau mbalimbali wa barabara pale JNICC kujadili miundombinu yetu ya jiji la Dar es salaam. Pia tumeandaa utaratibu ambao utawapatia fursa wananchi kutuma taarifa zao juu ya barabara zao kule wanakoishi na kama barabara ni mbaya mkandarasi wa eneo husika ataeleza sababu na akishindwa kueleza tutamtumbua. Barabara zetu zote za Dar es salaam zinatakiwa kuwa safi na zakuvutia,” alisema RC Makonda.

Mapema wiki hii RC Makonda akiwa katika kikao na Bodi ya Barabara, alisema kuwa hataki kuona kwenye mkoa wake barabara zinatengenezwa kwa gharama kubwa halafu zinaharibika kwa muda mfupi na kusababisha Kero kubwa kwa watumiaji wa Barabara.


RC aliwataka wajumbe wa bodi hiyo kuhakikisha wanazuia uharibifu wa barabara unaofanywa magari yanayobeba mizigo mikubwa kupita uwezo wa barabara.

Alisema katika bajeti ya serikali ya mwaka 2017 -2018 imetengwa zaidi ya shilingi Billion 184 kwaajili ya ujenzi wa barabara za mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni ongezeko la zaidi ya 5%.

Aidha Makonda aliziagiza makampuni zote zitakazofanya kazi ya ukamataji wa vyombo vya moto na kufanya kazi hiyo kinyume na mkataba hali inayoleta kero kwa wananchi kuvunja mikataba yao.

Hata hivyo Makonda amewataka watendaji hao kuhakikisha miradi yote iliyokusudiwa kutekelezwa na serikali inamalizika kwa wakati.

Katika kikao hicho kimejumuisha Wabunge, mameya, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wataalamu wa sekta ya barabara.