Wateja Wagoma Kujitokeza Katika Mnada wa Nyumba za Lugumi - MULO ENTERTAINER

Latest

9 Sept 2017

Wateja Wagoma Kujitokeza Katika Mnada wa Nyumba za Lugumi

Wateja Wagoma Kujitokeza Katika Mnada wa Nyumba za Lugumi
Mnada wa nyumba zinazomilikiwa na  Kampuni ya Lugumi Enterprises Limited zilizopo Mbweni na Mtaa wa Mazengo Upanga jijini Dar es Salaam  unafanyika leo Septemba 9.

Kampuni ya Udalali ya Yono  ipo  Mbweni JKT  kupiga mnada ghorofa mbili za kampuni hiyo ya Lugumi.

Akizungumza wakati wa Mnada huo Mkurugenzi wa Kampuni ya Yono Scolastica Kevela amesema nyumba ya kwanza  imefikia Shilingi 460 milioni lakini bado haijapata mteja.

"Wateja waendelee kujitokeza na tutabaki hapa hadi saa 12 jioni" amesema Kevela