Mama Samia Ahamia Rasmi Dodoma Leo - MULO ENTERTAINER

Latest

16 Dec 2017

Mama Samia Ahamia Rasmi Dodoma Leo

Mama Samia Ahamia Rasmi Dodoma Leo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ahamia rasmi mjini Dodoma leo. Baada ya Rais Magufuli kuagiza serikali ya Awamu ya tano kuhamia mjini humo.


Akizungumza mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Kilimani mjini Dodoma, Samia ameomba wananchi wa mkoa huo kuonyesha ushirikiano katika kufanya kazi ili kulisukuma gurudumu la maendeleo

"Nilikuwa hapa kwa muda mrefu kidogo lakini nilipangiwa kuhamia rasmi leo Desemba 15 na nimefurahi kwamba nitafanya kazi mahala pangu pa kazi pa kudumu," amesema Samia.

Amesema kauli mbiu yake kwa wakazi wa Dodoma ni kuufanya mji huo kuwa wa kijani hivyo Desemba 21 ataendesha mpango wa kupanda miti katika wilaya zote.

"Kwa kuwa nasimamia pia masuala ya mazingira nitaendesha zoezi hilo ili kurudisha hali ya Dodoma," ameongeza
.