Rayvanny Afunguka Kinachokwammisha Kolabo Yake na Derulo - MULO ENTERTAINER

Latest

16 Dec 2017

Rayvanny Afunguka Kinachokwammisha Kolabo Yake na Derulo


Rayvanny Afunguka Kinachokwammisha Kolabo Yake na DeruloMsanii wa muziki Bongo, Rayvanny amefunguka kinachokwamisha kolabo yake na Jason Derulo.

Muimbaji huyo wa WCB ambaye June 26 mwaka huu alionekana studio na Jason Derulo ameiambia The Base, ITV kuwa kazi hiyo ilishafanyika ile anasubiri Derulo aimalizee mixing kisha amtumie.

“Nilifanya ngoma kwenye studio yake lakini ratiba yake inakuwa imebana sana anakuwa anazunguka kwenye miji mingi tofauti, so akaniambia siwezi nikakutumia kitu ambacho hakijakaa proper subiri mpaka tuimix vizuri” amesema Rayvanny.

Hata hivyo Rayvanny ameeleza kuwa katika safari yake ya sasa ya Marekani ambapo ameenda kwa ajili ya ku-shoot video atafuatilia na hilo pia.