Amewataka watilie mkazo wimbo wa Taifa na nyingine zinazozungumzia ukombozi.
Mnangagwa amesema hayo katika mkutano wa chama hicho uliomvua uongozi rasmi aliyekuwa kiongozi mkongwe wa chama na Serikali ya Zimbabwe, Rais Robert Mugabe na kumtimua mkewe Grace.
Mkutano huo pia umemwidhinisha Mnangagwa kuwa mkuu mpya wa chama na mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2018.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Mnangagwa amewataka wanachama kutambua kuwa yeye ni Rais wa watu wote na wala si wa kikundi fulani.
Amesema huu si wakati wa kutambiana kuwa kundi gani limeshinda bali kila mwanachama anapaswa kuzingatia mahitaji ya wananchi ambao wanataka maendeleo.
Rais Mnangagwa amesema wanachama wanapaswa kurekebisha uchumi ikiwa wanataka wawe na nafasi ya kushinda uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.
"Tutashinda uchaguzi ikiwa tu tutaweza kuonyesha ishara kwamba tunafufua uchumi na wakati huohuo, tutaweza kupata mafanikio ya kiuchumi ikiwa tutaweza kuhakikisha tunashinda tena uchaguzi," amesema Mnangagwa.