Mwanamke Amuuza Mwanawe wa Siku Tatu Siku ya Mwaka Mpya - MULO ENTERTAINER

Latest

12 Jan 2018

Mwanamke Amuuza Mwanawe wa Siku Tatu Siku ya Mwaka Mpya



ITUI, KENYA: Mwanamke aliyejulikana kama Sarahi Kwamboka amepandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kumuuza mwanae wa siku 3 siku ya mwaka mpya kwa dau la Shilingi 10,000 za Kenya.
-
Mtuhumiwa huyo ambaye ni Mama wa Watoto 3 alipandishwa kizimbani pamoja na anayedaiwa kumnunua mtoto huyo, Bi. Bernadette Musanya.
-
Korti ilielezwa kuwa Mtuhumiwa huyo wa kwanza alijifungua mtoto wa kike aitwaye Fridah Mutheu katika kituo cha afya cha Kanyangi siku ya Desemba 29, 2017 huko Kitui na siku 3 baadaye yaani siku ya mwaka mpya ndipo alimuuza kwa Bi. Musanya.
-
Wawili hao walikubali mashtaka ambapo mama huyo alidai amefanya hayo kutokana na umasikini unaomkabili na aliona atashindwa kumlea mtoto huyo pamoja na watoto wake wengine wawili.