Zaidi ya watu 65 wamefariki kwa Joto kali la nyuzi joto 44 lililotanda mjini Karachi nchini Pakistan. wengi wakiishiwa nguvu haswa kipindi hiki cha Ramadhan ambapo wengi huwa hawali wala kunywa nyakati za mchana.
Faisal Edhi, mkuu wa Shirika la Edhi ambalo linafanya kazi za maadili na huduma ya wagonjwa nchini humo, ameviambia vyombo vya habari kwamba miili ya watu 114 waliletwa kwenye nyumba ya kuhifadhia maiti mjini Karachi katika siku tatu zilizopita na watu 65 kati ya walioletwa walifariki kutokana na kiharusi cha joto.
Mamlaka nchini Pakistan imewasihi watu wapunguze kutembea juani.