Jidanganye uoe Mwanamke mwenye Kazi. Asilimia kubwa wanarudi wamechoka kiasi kwamba hata mkilala hakugeukii wala hataki umguse. Atataka haki sawa eti akipika wewe ufue Nguo au umsaidie Kupika. Mara chache atakutengea Maji ya kuoga. Muda mwingi anatoka Kazini amenuna, hata akichelewa hataki umuulize alikua wapi.
Wana viburi sana, ukiwauliza kitu wanajibu kwa nyodo, hatakusikiliza. ukimsemesha kidogo tu ataenda kulala kwa marafiki zake au kwa ndugu zake. Haoni aibu kukukolomea Mwanaume hata mbele za watu. Anajifanya anawivu sana, atapiga Simu kila dakika kukuuliza ulipo as if wewe mtoto mdogo hujui pa kwenda.
Anapewa Mshahara lakini hautojua unaenda wapi kwani kila siku utaombwa hela ya Salon. Siku ukiishiwa ukamuomba hela ya Bia hatakupa bali atasema siwezi kukupa hela yangu ukahonge Malaya zako.
Siku akifurahi atakuletea zawadi ya Shati, mara moja kwa Miezi Mitano kana kwamba halipwi Mshahara. Dawasco wakimkuta hatawapa hela yake hata kama anayo, atawambia hayupo.
Ukioa Mwanamke mwenye kazi utamfaidi siku ukiumwa, ataomba ruhusa ili aje akuhudumie, atakununulia sana Socks na Matunda Matunda. akitaka kununua kitu atakua na kianzio sana sana ataomba umuongezee Hela.