Mbwana Samatta Noma..Aipeleka KRC Genk Europa League Usiku wa May 27 2018 - MULO ENTERTAINER

Latest

28 May 2018

Mbwana Samatta Noma..Aipeleka KRC Genk Europa League Usiku wa May 27 2018

Baada ya kusuasua katika mechi kadhaa kutokana na kutoka majeruhi nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta usiku wa May 27 2018 amerudi tena kwenye headlines.

Mbwana Samatta amerudi kwenye headlines tena baada ya kuanza katika kikosi cha KRC Genk kilichokuwa kinacheza game za Play Off ya kuwania kupata tiketi ya kucheza michuano ya UEFA Europa League kwa msimu wa 2018/2019 wakicheza dhidi ya Zulte-Waregem.

Mchezo huo KRC Genk walicheza wakiwa nyumbani na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0, Mbwana Samatta ndio alianza kuionesha Genk njia ya kueleka Europa League kwa kufunga goli la kwanza dakika ya 18 ya mchezo kabla ya Jere Uronen kufunga goli la pili dakika ya 28.

Ushindi huo sasa ni wazi unaipeleka KRC Genk kushiriki michuano ya UEFA Europa League ambapo kwa msimu wa 2018/19 itashirikisha pia timu za Chelsea na Arsenal za England, hata hivyo hiyo itakuwa fursa kwa Mbwana Samatta kucheza tena michuano hiyo kwa mara ya pili baada ya kucheza kwa mara ya kwanza msimu wa 2016/2017.