NYOTA inaendelea kumuwakia beki kiraka wa Simba, Shomari Kapombe kwani sasa taarifa zinasema anatakiwa na moja ya timu iliyopanda kucheza Ligi Kuu ya Hispania msimu ujao.
La Liga ni ligi kubwa Ulaya ambapo mastaa mbalimbali wanacheza wakiwemo Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya Simba, kimelipasha Championi Jumamosi kuwa, kuna timu kubwa kutoka Hispania ambayo imepanda ligi kuu inamtaka Kapombe alipokuwa akiichezea Simba mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry ya Misri baada ya kuvutiwa na uwezo wake.
Championi Jumamosi lilimtafuta Kapombe ili aweke wazi kuhusiana na taarifa hizo, ambapo alisema: “Nikweli kuna mawakala zaidi ya watatu wamenipigia hivi karibuni wakinitaarifu uwepo wa timu zaidi ya tatu kunihitaji.”
“Wakala wa kwanza ameniambia kuna timu ya Hispania inanitaka, lakini pia zipo zingine mbili, moja kutoka Urusi na nyingine ipo Bara la Asia ambazo zote nimeshataarifiwa kunihitaji, hivyo wakala wangu ameniomba nitume tu baadhi ya ‘clip’ (video) zangu ili aweze kukamilisha dili hilo.
“Hii ni bahati sana kwangu kuonekana kwa muda mfupi huu ambao nimecheza Simba, japo nia yangu ningependa kuendelea kuwa hapa ili nijiweke vizuri zaidi kwani nina malengo mengi sana ambayo bado sijayafikia pamoja na kwamba wao wameshaona uwezo wangu,” alisema Kapombe.
Stori: Musa Mateja, Dar es Salaam
27 May 2018
New
Mchezaji Kapombe Kucheza Ligi Kuu Hispania Msimu Ujao
mulo
Newer Article
Cheo cha koplo, Pingu vyamtia mbaroni mhudumu wa hoteli
Older Article
Diamond Platnumz Apewa Gari Mpya na Uongozi wake wa Wasafi
Atletico Madrid 'Yamfukuza' Diego CostaApr 27, 2019
Uganda Watuma Salamu kwa Taifa StarsMar 23, 2019
Labels:
Michezo