Mwanamuziki Mrisho Mpoto amesema moja ya sababu iliyopelea kuandika wimbo wake mpya ‘Nimwage Radhi’ ni baada ya kuona mtindo wa wasanii maarufu Bongo kuoa nje ya nchi.
Kauli ya Mpoto amekuja pale alipoeleza kuwa awali alishauriwa na Harmonize video hiyo ikafanyike Nigeria au Afrika Kusini ila akakataa kutokana ujumbe wa wimbo huo ni kwa ajili ya Watanzania.
“Kwa sababu wimbo mimi naongea na Watanzania, nilikuwa nimeguswa na jinsi vijana wetu wa Kitanzania wanavyokwenda kuoa nje ya Tanzania, kwa nini vijana wetu maarufu hawataki kuoa nyumbani?,” alihoji.
“Nikaliona hilo, nikajua kuna tatizo hapa, hawa wanahitaji kufundwa, hawa kuna maneno wanatakiwa kuambiwa, waambie na mwenye maneno yake,” Mpoto ameiambia Times FM.
Katika hatua nyingine amesema kuwa licha ya video hiyo kufanyika Bongo, pia Harmonize amechangia karibia asilimia 40 ya bajeti yake na sehemu iliyobaki akamalizia yeye pamoja na wadau.
28 May 2018
New