Mwanamke Ashikiliwa na Polisi Baada ya Kumnyesha Mkojo Mtoto wake wa Kambo - MULO ENTERTAINER

Latest

27 May 2018

Mwanamke Ashikiliwa na Polisi Baada ya Kumnyesha Mkojo Mtoto wake wa Kambo


Mkazi wa Mtaa wa Shede anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumnywesha mkojo mtoto wake wa kambo mwenye miaka 9 kama adhabu baada ya kujisaidia haja ndogo kitandani akiwa amelala

Kwa mujibu wa maelezo ya mtoto huyo anasema mama yake wa kambo huyo alienda kumuamsha na kumkuta amejikojelea, alimpiga na baada ya kipigo alikojoa kwenye kopo na kumpa anywe

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa, Bethnsimbo Shija alisema mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na atafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi wa awali kukamilika

Mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa anasoma darasa la tatu katika moja ya shule za msingi mkoani humo na alipewa adhabu hiyo Mei 23 mwaka huu - #regrann