Uongozi wa klabu ya Coastal Union ya Tanga umesema umejiandaa vilivyo kuelekea mechi ya leo dhidi ya African Lyon.
Kocha Mkuu wa timu, Juma Mgunda, amesema wapo tayari kupigania alama tatu mbele ya watoto wa Dar es Salaam Lyon ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kupigania ubingwa wa ligi.
Mgunda amesema timu hiyo ina jumla ya wachezaji 30 ambao wote wapo fiti kuelekea kibarua hicho kitakachopigwa majira ya saa jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Aidha, Mgunda amesema kuwa mchezaji Ali Kiba ni moja ya wachezaji ambao waliopo kwenye kikosi na akieleza kuwa kama Mungu atajaaliwa uzima atacheza mechi hiyo.
Kiba ambaye ni Mwanamuziki mkubwa Tanzania na Afrika Mashariki pamona na Afrika kwa ujumla alijiunga na Coastal Union kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja ambapo mpaka sasa hajacheza mchezo wowote.