Mwaka 1987 Dr.Ben Carson alitengeneza historia ya kipekee kwa kuwa daktari wa kwanza aliyefanikisha kuwatenganisha MAPACHA waliokuwa wameungana kwenye sehemu ya nyuma ya vichwa vyao (Visogoni)
Upasuaji wa aina hii HAUJAWEZA kufanikisha tena kuwafanya watoto wote waendelee kuishi baada ya kutenganishwa tangu Dr.Ben alipofanikiwa.Mara nyingi mtoto mmoja wao hupoteza maisha ama wote kwa pamoja.Upasuaji huu ulijumuisha timu ya madatari 50 wakiongozwa na Dr.Ben Carson na ulichukua saa 22 mpaka kukamilika kwake.
Picha ya juu inawaonesha mapacha hao wakiwa bado watoto wachanga walioungana,picha ya chini ikiwa imepigwa miaka 31 tangu watenganishwe na kila mmoja kuanza kuishi maisha yake binafsi.