Hukumu ya Msanii Baba Levo Kutolewa Leo - MULO ENTERTAINER

Latest

19 Sept 2018

Hukumu ya Msanii Baba Levo Kutolewa Leo

Hukumu ya Msanii Baba Levo Kutolewa Leo

Hatma Msanii wa Bongo fleva na diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini (ACT) Crayton Chipando maarufu kama Baba Levo anayekabiliwa na kesi ya kumshambulia muuguzi itajulikana leo hukumu itakapotolewa mjini Kigoma.

Baba Levo amefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mjini Kigoma leo kusikiliza hukumu ya kesi inayomkabili.

Diwani huyo anakabiliwa na mashtaka matatu ya kushambulia, vurugu na lugha ya matusi dhidi ya muuguzi wa zahanati ya Msufini, Christina Gervas.

Msanii huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 12 . Kesi hiyo namba 62 ya mwaka 2018 ilikuwa ikisikilizwa kwa Hakimu Mfawidhi Flora Mtalania, huku msanii huyo akitetewa na wakili Thomas Msasa.