Mbunge Sugu Aibua Mazito Mbeya - MULO ENTERTAINER

Latest

20 Sept 2018

Mbunge Sugu Aibua Mazito Mbeya

MBUNGE wa Jimbo la Mbeya mjini,  Joseph Mbilinyi  ‘Sugu’ (Chadema),  ameibua madai mazito kwamba aliyekuwa mgombea udiwani kata ya Maanga,  Steven Mwashilindi,-

alipigwa kofi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji, James Kasusura, baada ya kukataa kusaini kukubali kushindwa kwa madai kwamba matokeo hayo yalikuwa 'feki'.

Akizungumza kwenye ofisi za Kanda ya Nyasa, ‘Sugu’ alisema mgombea huyo alipigwa makofi baada ya kugoma kusaini matokeo aliyodai kuwa ni feki.

“Mgombea  wetu alipigwa makofi na mkurugenzi wa jiji baada ya kukataa kusaini matokeo feki kwenye chumba cha kuhesabia kura,” alisema Sugu.

Naye Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, Mch. Peter Msigwa, alisema kuwa kinachofanyika  kwenye chaguzi hizo hakiumizi tu wapinzani bali hata wananchi.

Alisema siasa hizo haziikomoi Chadema akiwamo ‘Sugu’ au Freeman Mbowe, bali kinaondoa nguvu ya umma  ya  kuchangua mtu wanayemtaka, na kuomba Serikali kuendelea kuienzi demokrasia ya kweli.

Aliyekuwa mgombea wa udiwani Kata ya Maanga  aliyedaiwa kupigwa kofi na Mkurugenzi, Steven Mwashilindi, alikiri kupigwa baada ya kugoma kusaini kwenye chumba cha kuhesabu kura.

Alieleza kuwa alikataa kusaini fomu ya matokeo baada ya kuona sehemu anayoelezwa siyo sahihi na kudai kuwa aliondoka.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Jiji, James Kasusura, alikanusha kumpiga kofi mgombea huyo.

Alisema   kwenye kituo cha kuhesabia kura kulikuwa na waandishi nane mlangoni walikuwa zaidi ya sita kama kungekuwa na tukio la kupiga wangepata picha nzuri za kuuza kwenye magazeti.

“Nawahakikishia tukio la kupigwa mgombea halikuwepo, mgombea alishuhudia kura zikihesabiwa, wametunga nadhani ni muondelezo wao wa chuki tangu kipindi cha kampeni,” alisema Kasusura.