Rais JPM Amteua Ali Idi Siwa Kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini NSSF - MULO ENTERTAINER

Latest

20 Sept 2018

Rais JPM Amteua Ali Idi Siwa Kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini NSSF

Rais JPM Amteua Ali Idi Sa=iwa Kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini NSSF
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amefanya uteuzi Balozi mstaafu Ali Idi Siwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi wa Siwa unaanza rasmi leo Septemba 20, 2018.

Kabla ya uteuzi huo Siwa alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda ambapo amehudumu kwa miaka minne kuanzia mwaka 2014 alipoteuliwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mpaka Machi 2018 ambapo alistaafu.

Ikumbukwe kuwa Julai 24 katika mkutano wake na wanahabari, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Jenister Mhagama, alivunja Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) huku akisema taratibu za uteuzi wa bodi mpya zitakamilika baada ya muda mfupi.