Muungano wa Vyama vya Upinzani Burundi Wameguka - MULO ENTERTAINER

Latest

13 Sept 2018

Muungano wa Vyama vya Upinzani Burundi Wameguka

Muungano wa Vyama vya Upinzani Burundi Wameguka
Mwanasiasa mkongwe na mashuhuri wa upinzani nchini Burundi, Agathon Rwasa amejiengua katika muungano wa vyama vya upinzani nchini humo na yumo mbioni kusajili chama kipya cha siasa.

Katika mkutano na wafuasi wake wasiopungua 500 kutoka mikoani ,wamewakilisha mapendekezo mbalimbali kwa mujbu wa sheria ili wafikishe maombi yao kwenye wizara ya mambo ya ndani kwa usajili wa chama chao cha National Liberty Front Amizero y'Abarundi.

Rwasa amesema itawalazimu wanasiasa wa upinzani kujidhatiti katika vyama vyao ili baadae kujiweka pamoja wakati wa mpambano wa uchaguzi kwa mujibu wa katiba mpya.

Pia amewataka wafuasi wake kuwa watulivu,wavumilivu na kuchangia kwa hali na mali toka sasa hivi hadi itapofikia uchaguzi mkuu miaka miwili ijayo.

Kwasasa Rwasa ni Makamu Spika wa Bunge akiwakilisha mseto wa vyama vya upinzani wa amizero y'abarundi.

Muungano huo katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2015 ulishika nafasi ya pili ukitanguliwa na chama tawala CNDD FDD cha Rais Pierre Mkurunziza.

Rwasa amewataka wafuasi wake kuwa watulivu,wavumilivu na kuchangia chama kipya kwa hali na mali toka sasa hivi hadi itapofikia uchaguzi mkuu miaka miwili ijayo.
Rwasa amewahi kuishi uhamishoni katika nchi jirani ya Tanzania kwa takribani miaka 20 alipotoroka uongozi wa watutsi wachache.

Mazungumzo ya Amani ya Arusha yaliwawezesha wana siasa wa kabila kubwa la wahutu kurejea nyumbani. Agathon Rwasa alitoroka tena mchi mwaka 2010 wakati CNDD FDD ikiongoza. Baadae alirejea Burundi 2013.

Alijiunga na bunge baada ya uchaguzi wa 2015 ulio susiwa na upinzani. Iwapo chama chake kitasajiliwa ,anasadikiwa kuwa mpinzani mkubwa kuliko wengine dhidi ya chama tawala CNDD FDD.