Zaidi ya miili ya watu 74 yakutwa katika kaburi moja nchini Libya - MULO ENTERTAINER

Latest

13 Oct 2018

Zaidi ya miili ya watu 74 yakutwa katika kaburi moja nchini Libya

Zaidi ya miili ya watu 74 yakutwa katika kaburi moja nchini Libya
Kaburi lenye miili ya watu 75 limegunduliwa nchini Libya. Miili hiyo inashukiwa kuwa ya wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS. Maafisa  nchini Libya wamegundua kaburi lililozikwa watu wengi linaloaminika kuwa na miili 75 ya wapiganaji  wa  kundi  la  Dola  la  Kiislamu  karibu  na  mji wa  pwani  wa  Sirte, ambao  hapo  zamani  ulikuwa ngome  kuu  ya  kundi  hilo  la  itikadi  kali  katika  Afrika Kaskazini.

Msemaji wa jeshi la nchi hiyo katika  eneo  la Benghazi , Salem el-Ameel , amesema  mkaazi  mmoja aliripoti  kuhusu  kaburi  hilo  kiasi ya mwezi mmoja uliopita  katika  shamba  katika  wilaya  ya  al-Daheir, mashariki  mwa  Sirte.



Ameongeza  kwamba  wale waliopatikana  katika  kaburi  hilo  wanaonekana  kuwa wamevaa  nguo  za  wapiganaji  wa  IS, lakini  uchunguzi wa  kitaalamu  unahitajika  kubaini  wao  ni  nani  na wanatoka  wapi.

Katika tukio  jingine, jeshi  hilo linalojitambulisha  kuwa  jeshi  la  taifa  la  Libya  limesema limekamata  meli  mbili  za  uvuvi  za  Italia  katika  pwani ya  Libya.