Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars usiku wa October 12 2018 ilikuwa Cape Verde kucheza mchezo wake wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika mwakani 2019, huo ukiwa mchezo wao wa tatu wa Kundi lao.
Taifa Stars wakiwa ugenini waliruhusu magoli mawili ya mapema kiasi ambacho yalipelekea umakini kupungua na Cape Verde kutawala mchezo zaidi, hadi dakika 90 zinamalizika Taifa Stars walimaliza game kwa kupoteza kwa magoli 3-0.
Magoli ya Cape Verde yakifungwa na Ricardo Gomes dakika ya 16 na 24 na Stopira dakika ya 85, ushindi huo umeifanya Cape Verde iongoze Kundi kwa muda ikisubiri matokeo ya Uganda na Lesotho na Cape Verde wamefikisha jumla ya point nne sawa na Uganda wakitofautiana magoli.
Taifa Stars sasa imebakiza michezo mitatu kati ya sita iliyocheza na itarudiana na Cape Verde October 16 2018 uwanja wa Taifa Dar es Salaam, kundi lao hadi sasa timu zote nne zina nafasi ya kufuzu michuano hiyo.