Shilole Atoa Onyo Kali Kwa Wanawake Wanao Anza Kumtamani Mume Wake...Kisa Kawa Handsome - MULO ENTERTAINER

Latest

9 Jan 2019

Shilole Atoa Onyo Kali Kwa Wanawake Wanao Anza Kumtamani Mume Wake...Kisa Kawa Handsome


Msanii wa muziki Bongo, Shilole amechimba mkwara kwa wale wote anaoamini kuwa wanamnyemelea mume wake, Uchebe.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa toka mwanzo aliridhika na hali ya mume wake lakini sasa watu wanapoona anang'aa ndipo wanamnyemelea. Kupitia ukurasa wake Instagram ameandika;

"Nililizika na hali yako tangu mwanzo mpaka sasa unashaine Ila wadangaji msivyo na haya mnaanza
kumwambia Mume wangu Uchebe Umekuwa Handsome, Mkome Namtunza! zamani mlikuwa wapi??," ameeleza Uchebe.

Shilole na Uchebe walifunga ndoa December 07, 2017 na mwaka jana Uchebe alioonekana kwenye video ya muimbaji huyo inayokwenda kwa jina la Mchakamchaka.