CCM Yamtaja Atakayegombea Urais Mwaka 2020 - MULO ENTERTAINER

Latest

9 Jan 2019

CCM Yamtaja Atakayegombea Urais Mwaka 2020


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa alichokifanya Rais Magufuli kwa kipindi hiki kifupi alichokaa madarakani, ni dhahiri kuwa hakuna mwingine atakayepewa ridhaa na chama zaidi yake kugombea 2020.


Polepole ametoa kauli hiyo leo katika kipindi cha East Africa BreakFast cha East Africa Radio ambapo amesema CCM haina sababu ya kupitisha mgombea mwingine ikiwa Rais Magufuli amefanya vitu vikubwa na bado uwezo na nguvu ya kulitumikia taifa bado anao.


"Mwaka 2020 hatuna shaka katika nafasi ya Urais mgombea wetu ni Rais Magufuli hatuna wasiwasi kabisa na kiongozi wetu kwa aliyofanya kwa kipindi hiki njia ni nyeupe, lakini hatujakataza wengine kuchukua fomu wao wachukue tu", amesema Polepole.


Akizungumzia kupunguzwa kwa wanachama wanaotakiwa kupiga kura za maoni amesema kuwa, "Sisi hatuukatai ubaya ambao ulikuwepo zamani, tunakiri na kufuta kwa kufanya mema, CCM tuna kadi za kielektroniki hivyo huwezi kupiga kura ya maoni, kama huna kadi ile na sio kwamba tumewapunguza bali ni mabadiliko ya teknolojia hivyo wahakikishe wanakubaliana na mabadiliko na hakuna aliyefukuzwa".


Aidha Polepole amesema kuwa chama chake, hakipokei tena watu wanaotoka upinzani wao wabaki hukohuko usajili umeshafungwa, na kudai kuwa waliobaki hawana vigezo na wajiandae kuachia majimbo 2020.