Askari Watano Wapewa Zawadi Ya 1,500,000 Baada Ya Kukataa Rushwa Kutoka Kwa Wachina Wamiliki Wa Mashine Za Kamali - MULO ENTERTAINER

Latest

23 Feb 2019

Askari Watano Wapewa Zawadi Ya 1,500,000 Baada Ya Kukataa Rushwa Kutoka Kwa Wachina Wamiliki Wa Mashine Za Kamali

Askari Watano Wapewa Zawadi Ya 1,500,000 Baada Ya Kukataa Rushwa Kutoka Kwa Wachina Wamiliki Wa Mashine Za Kamali

Askari watano mkoani Dodoma wamepewa zawadi ya Tsh.Milioni Moja na Nusu kutoka kwa ofisi ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa baada ya kukataa rushwa ya Tsh.Milioni 1 Kutoka kwa Wamiliki wa Mashine za kuchezea kamali Raia wa China.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Februari 22,Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Murroto  amewataja askari waliopewa Motisha hiyo ili waendelee kuchapa kazi zaidi ni Inspekta Ntilungila,F 3129 Coplo Edward,G 2856 D/C  Ahmed,G 1973 D/C Edward na wa tano ni askari mwenye No.G 6593 PC Stanley.

Raia wa Kichina waliokamatwa wakitaka kutoa hongo hiyo ni Chen Xian Wen[35],Chen Ji[21] na Mwingine ni Lin Bibi[30].

Kamanda Murroto ameendelea kufafanua kuwa ,Jeshi la polisi Mkoa wa Dodoma limefanikiwa kukamata jumla ya watuhumumiwa  wa makosa mbalimbali 49 pamoja na  mali mbalimbali za wizi zikiwemo mashine za kuchezea kamali 138.

Katika wilaya ya Dodoma, Zimekamatwa Jumla ya mashine  za kamali 77 na watuhumiwa 12  wakiwemo Raia wa china na kusema kuwa  Raia hao wa china ndio wamiliki  na wasambazaji wakuu wa mashine hizo ambapo wakati wanakamatwa  walikutwa na mashine  62 wakiwa wamezificha  baada ya kupata taarifa ya kuwepo msako mkali  wa mashine hizo.

Pia, Muroto amesema kuwa vijana wengi wamekuwa wakicheza michezo hiyo ambapo wao ndio nguvu kazi ambayo inatakiwa kuwa kazini na kuwataka Vijana kuchangamkia fursa zilizopo Jijini Dodoma na kuachana na Vitendo hivyo .

Aidha Kamanda Murroto amesema kuwa wamekamata mafurushi yenye nguo mbalimbali wanazotumia watalii kupandia Mlima Kilimanjaro .

Vifaa hivyo ni pamoja na makoti ambayo yaliiibwa Kilimanjaro na kuanza kusafirishwa kupitia Gari La Machame.

Vilevile Kamanda Muroto amesema  tarehe 20/2/2019 wilayani Chamwino Mkoani Dodoma alikamatwa Tumaini Makali [28]mkazi wa kijiji cha Mahama tarafa ya Chilonwa wilayani Chamwino akiwa na Dawa za kulevya  aina ya bhangi kete 93 yalikuwa yamehifadhiwa kwenye mfuko wa nailoni maarufu RAMBO  akiwa anauza nyumbani kwake.

Tukio jingine ni MICHAEL TANDALA na wenzake 8 wote wakazi wa kijiji cha Mvumi  wilayani Chamwino walikamatwa wakiwa na bangi kavu kg 2 pamoja na mbegu.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt Binilith Mahenge amelipongeza jeshi la polisi la mkoa wa Dodoma linaloongozwa na kamanda muroto kwa kazi kubwa wanayo ifanya pamoja na kupiga marufuku kwa nyumba yeyote ya mtu Binafsi kuwa na mashine hizo.

Katika hatua nyingine Dkt Mahenge amewataka wazazi kuwafuatilia watoto wao ili wasijiingize katika vitendo ambavyo si salama kwao.

Mbali na hilo Kamanda muroto amesema katika wilaya ya chamwino  Mkoani Hapa  amekamatwa  Tumaini  Makali (28) mkazi wa kijiji cha Mahama  Tarafa ya Chilonwa , Wilayani Chamwino akiwa na madawa ya kulevya yadhaniwayo kuwa ni Bhangi  kete 93 ambayo yalikuwa yamehifadhiwa  kwenye mfuko wa nailoni  maarufu kama Rambo, akiwa anayauza nyumbani kwake.    

Hatahivyo,  Kamanda Muroto amesema kuwa jeshi la polisi litawachukulia hatua wale wote watakao kamatwa kwa kushawishi  kutoa rushwa au kupokea rushwa kutoka kwa mtu yeyote Yule