Klabu ya Real Madrid imekubali kichapo cha goli 2-1 kutoka kwa Girona kwenye uwanja wao wa Santiago Bernabeu mapema jioni ya leo.
Kwenye mchezo huo wa mzunguuko wa 24 wa La liga, Madrid kwa sasa wamepoteza mechi saba za Ligi hiyo ya Hispania.
Girona wamepata magoli hayo kupitia kwa washambuliaji wake Cristhian Stuan na Portu, huku Madrid goli lao likifungwa na Casemiro .
Katika mchezo huo, mtukutu Sergio Ramos amelimwa kadi nyekundu na kuweka historia kuwa mchezaji wa kwanza kufikisha kadi nyekundu 20 katika Ligi kuu ya hispania (La liga) kwa muda wote.
Katika michuano yote, Ramos ana jumla ya kadi 25 nyekundu na ndiye anayeongoza kuwa na kadi nyingi kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.