Baada ya kupoteza mchezo wa pili katika Ligi Kuu Bara wanachama wa Yanga wameilalamikia Bodi ya Ligi ya TFF kwa kuchelewesha kutangaza majina ya waamuzi wa mechi ya watani.
Mwanachama anayefahamika kwa jina la Abdallah Chitemo, amesema Bodi ya Ligi inapaswa kumtangaza Mwamuzi walau siku 6 kabla kuelekea mechi hizo.
Chitemo amefunguka kuwa yawezekana kukawa na njama zinapangwa ili kuwaharibia Yanga makusudi kutokana na Bodi hiyo ya Ligi kuchelewesha utangazaji wa Mwamuzi.
Ameeleza kuwa katika nchi zilizoendelea Mwamuzi hutangazwa mapema zaidi na akiwataka Bodi kujitathmini upya ili kuepuka lawama zisizo na msingi.