Polisi Tanzania kuajiri askari wapya 3,000 - MULO ENTERTAINER

Latest

13 Aug 2021

Polisi Tanzania kuajiri askari wapya 3,000

 



JESHI la Polisi nchini Tanzania, limeajiri askari polisi wapya zaidi ya 3,000. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana Alhamisi tarehe 12, Agosti 2021 na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro akifunga mafunzo ya uongozi mdogo cheo cha Sajenti wa Polisi, katika Chuo cha Polisi Zanzibar

“Jana wakati najiandaa kuja hapa nimetoa ajira takribani 3,000 za askari wapya. ajira 3000 na kitu si jambo dogo. Takribani miaka mitano tulipata ajira 800, lakini sasa tumepata ajira zaidi ya 3,200 na kitu,” amesema IGP Sirro.

IGP Sirro amewataka Askari Polisi kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, na kujiepusha na vitendo vya kuonea wananchi.


 
“Tumepewa dhamana kuhakikisha uhalifu unapungua, ni aibua sana unasimaia sheria unakuwa wa kwanza kuvunja sheria. Kwa vile tupo kwa mujibu wa sheria, tuzimize wajibu wetu kwa mujibu wa sheria. Tusimuonee Mtanzania kwa maslahi yetu binafsi, tuwatendee haki Watanzania,” amesema IGP Sirro.

Aidha, IGP Sirro amewataka Polisi kuwashughulikia watu wasiotii sheria za nchi.

“Tusimuonee Mtanzania kwa maslahi yetu binafsi, tuwatendee haki Watanzania. Lakini wale ambao sio wazalendo wa nchi hii, wale wanaotaka kuleta uvunjifu wa amani tuwashughulikie vizuri kwa mujibu wa sheria,” amesema IGP Sirro.