New
Mwigizaji mkongwe wa filamu hapa Bongo, Yvonne Cherly ‘Monalisa’ (33) amesema kuwa yeye siyo gubegube kwani alishawahi kukaa ndani ya ndoa lakini sasa ameamua kutulia.
|
Yvonne Cherly ‘Monalisa’ |
Akipiga stori mbili-tatu na Gazeti la Uwazi, Monalisa alisema kuwa hata kama akiamua kurudi upya kwenye ndoa anaweza na kutilia msisitizo kuwa mwanaume atayemuoa lazima atambue kuwa anayemuoa ni Yvonne Cherly na si Monalisa kwani jina hilo litakalokuwepo kwenye cheti cha ndoa.“Mimi si gubegube, nikiamua kurudi na kufunga ndoa naweza tena nitaolewa kama Yvonne Cherly kwani ndilo jina langu halisi. Ninachokiwaza kwa sasa si kukaa ndani ya ndoa bali namna kazi zangu zitakavyoweza kuonekana zaidi,” alisema Monalisa.