Mtumishi Fredrick Kishindo ‘Badoo’ Akijitetea
Ilikuwaje?
Awali chanzo cha habari kilichoomba hifadhi ya jina lake kilieleza kuwa, Januari 11, mwaka huu Muinjilisti huyo anayesifika kwa kuhubiri watu waache dhambi alionekana akinyata kuingia kwenye nyumba ya mke wa mtu huyo iliyopo Sinza jijini Dar huku kukiwa na taarifa kuwa, mume wa mwanamke huyo alikuwa safarini.
Wifi mtu atonywa
Ikaelezwa kuwa, kufuatia mazingira hayo wifi wa mwanamke huyo alitonywa juu ya taarifa za Badoo kuingia kwenye nyumba ya kaka yake, maelezo yaliyomshitua hivyo kulazimika kuelekea eneo la tukio.
Baada ya wifi mtu huyo kufika nyumbani kwa kaka yake na kuhakikishiwa kuwa Badoo yuko ndani, aliuliza namna ya kuwapata makamanda wa Operesheni Fichua Maovu ya Global Publishers ‘OFM’ ambapo mmoja wa majirani alimpatia namba ya simu, akawapigia.
Polisi washirikishwa
Katika kuhakikisha usalama katika eneo hilo, wifi huyo pia aliwasimamisha polisi waliokuwa doria na kuwatonya juu ya uzinzi unaofanyika nyumbani kwa kaka yake na kwa kuwa kazi ya askari ni kulinda raia na mali zao, walitoa ushirikiano.
OFM watinga eneo la tukio
Baada ya makamanda wa OFM kupigiwa simu na kunyetishiwa juu ya uwepo wa Muinjilisti huyo chumbani na mke wa mtu, kwa kutumia pikipiki zao ziendazo kasi walianza safari na baada ya dakika chache walikuwa wamefika kwenye nyumba hiyo na kuwakuta polisi.
Muinjilisti, mke wa mtu live
Polisi wakiwa na OFM waliongozwa na wifi mtu huyo hadi kwenye chumba ambacho madhambi yalikuwa yakitendeka, walipoingia walikuta mke wa mtu na mtumishi huyo wa Mungu wakiwa kama walivyozaliwa.
Aibu iliyoje!
Baada ya kuona ‘picha imeungua’, mtumishi huyo alisikika akisema kuwa amepata aibu ambayo hakuitarajia huku akiomba asipigwe picha wala kufanyiwa kitendo kibaya bali apewe nafasi ya kujitetea.
Aidha mke wa mtu aliyenaswa akimsaliti mumewe alionekana kutahayari na aliishiwa nguvu zaidi alipomuona wifi yake aliyekuwa amefura ile mbaya.
Utetezi wa mtumishi wa Mungu
Kufuatia kunaswa huko, Badoo alijitetea kwa kujichanganya, awali alisema aliitwa na mwanamke huyo kwa ajili ya kuongea mambo ya biashara na kwamba eti walivua nguo kutokana na hali ya joto iliyokwemo chumbani humo.
Kana kwamba alihisi kajichanganya, Muinjilisti huyo aligeuza utetezi na kusema aliingia majaribuni baada ya kushawishiwa na ibilisi kisha mwanamke huyo hakumwambia kuwa ana mume.
Bofya hapa usikie utetezi wake
“Jamani naomba mnisamehe, si kosa langu bali ibilisi ndiye aliyenishawishi na huyu mwanamke hakuniambia kama ana mume. Hapa aliniita kwa ajili ya biashara flani.
“OFM nawajueni lakini niko chini ya miguu yenu, naomba msiitoe habari hii gazetini kesho n’tawaletea chochote pale ofisini kwenu, si ni pale Bamaga ee, napajua sana pale”.
OFM ni mwiko kupokea rushwa
Licha ya utetezi wake huo, makamanda wa OFM walisimamia weledi wa kazi yao na kumweleza kuwa, rushwa kwao ni mwiko hivyo kama atafika ofisini kwao iwe ni kwa ajili ya maelezo zaidi ya kwa nini amevunja moja ya amri kumi za Mungu.
Mpaka OFM wanaondoka eneo la tukio, mke wa mtu huyo alikuwa akiendelea kumuomba msamaha wifi yake huku Muinjilisti naye akijaribu kutuliza mambo yasifike mbali akidai kuwa, mke wake, ndugu na marafiki wakijua ataaibika.