Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Serikali ya Msumbiji imetoa tahadhari ya hali ya juu kwenye eneo la kaskazini na katikati mwa nchi hiyo kufuatia mafuriko yaliyotokana na mvua hizo.
Hadi sasa watoto 18 hawajuliani walipo na kuna taarifa watu kadhaa wamesombwa na maji yaliyokuwa yakitiririka katika mto mmoja.
Mawasiliano ya barabara inayounganisha eneo la kati na kaskazini mwa nchi hiyo yameharibika.