Waziri wa mambo ya ndani, nchini humo, Mathias Chikawe amesema kwamba msako wa kitaifa utaanza hivi karibuni kuwakamata waganga hao na kuwafikisha mahakamani ikiwa wataendelea na kazi zao.
Watu wenye ulemavu wa ngozi, wanakabiliwa tisho kubwa juu ya maisha yao, kwani wamekuwa wakilengwa kwa sehemeu zao za mwili na waganga pamoja na wapiga ramli wanaoamini kwamba viungo hivyo huleta bahati ya kupata mali.
Chama cha maalbino nchini humo kimesifu uamuzi wa serikali kuwapiga marufuku waganga hao.
"ikiwa kutakuwepo ushirikiano kati yetu na serikali, itakuwa ndio mwanzo wa nguvu mpya ya kupambana na ukatili unaotendewa walemavu wa ngozi,'' alisema mwenyekiti mmoja wa chama hicho Ernest Njamakimaya.
"ninaamini hii ndio njia ya pekee ambayo tunaweza kutumia kupambana na ukatili huo na kuukomesha kabisa.''
'ushahidi unavyovurugwa''
Zaidi ya watu 33,000 nchini Tanzania wanaaminika kuwa na ulemavu wa ngozi.
Kati yao sabini wameuawa katika miaka mitatu iliyopita lakini ni washukiwa kumi pekee wa mauaji hayo waliouawa.
Bwana Chikawe alisema kwamba msako wa kuwakamata na kuwashitaki waganga wa kienyeji itaanza katika kipindi cha wiki mbili zijazo katika eneo la Kaskazini mwa TZ, hasa mikoani Mwanza, Geita, Shinyanga, Simiyu na Tabora, ambako mashambulizi mengi dhidi ya maalbino yanafanyika.
Marufuku hio imewekwa kutokana mapendekezo ya jopo maalum ya pamoja kati ya polisi na waetetezi wa Albino.
Kazi ya jopo hilo sasa itakuwa kudadisi kesi zilizowahi kufikishwa mahakamani kuhusu mauaji ya Albino ili kutafuta ushahidi mpya pamoja na kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na kinachowashinikiza washambuliaji kutenda uhalifu huo.
Wadadisi wanasema baadhi ya kesi zilizowahi kuwasilishwa kuhusiana na mauaji ya Albino ziliporomoka kutokana na ukosefu wa ushahidi.