Exclusive: Jay Dee afunguka, atoa sababu za kuitosa ndoa yake na Mtangazi Gadner G Habash - MULO ENTERTAINER

Latest

13 Feb 2015

Exclusive: Jay Dee afunguka, atoa sababu za kuitosa ndoa yake na Mtangazi Gadner G Habash

SWALI: Tunasikia umeachana na mume ni kweli au uzushi?

JIBU : 
Hatujaachana niliamua kumuacha

SWALI: Kwanini umeachana/umemuacha mume?

JIBU : Nimemuacha kutokana na kuwa Ndoa inatakiwa iwe na maelewano, furaha, amani na upendo, ila kwa bahati mbaya vyote hivyo havikuwepo, sikuwa tayari kuendelea kuishi kwa maumivu huku niki pretend ili kuiridhisha jamii.

SWALI: Huoni kama umejishushia heshma kuachana na mume?

JIBU : Sioni hivyo, ila naona nilikuwa najishushia heshima zaidi kuishi na mume asie na heshima, anaeweza kutongoza na kushika wanawake makalio wakati mi niko jukwaani naimba. Kuwapa mademu magari yangu waendeshe na kuyagonga wakati niko safarini.

Ukiachilia mbali vipigo. Kutembea na wahudumu wa restaurant yangu. Ushahidi ninao; niliwahi mkuta anawashika mapaja na akakiri kosa. Bado kupigana na kuwatusi wateja pia. Kifupi ilikuwa ni ndoa ya mateso!

SWALI: Baada ya kuachana unategemea kuolewa tena?

JIBU : Ni mapema kujihakikishia uolewaji mwingine, ila haimaanishi kuwa sitopenda tena. Nahitaji kuwa makini zaidi Kuchagua mtu sahihi wa kumpa moyo wangu.

SWALI: Kwanini usirudiane na mumeo?

JIBU : Siwezi kurudi nyuma tena, huwa nina misimamo thabiti. Mpaka kuamua kuondoka na uvumilivu nilionao mjue ni maji ya shingo. When i say never, I mean Never.

SWALI: Uliwezaje kuishi na mume mlevi namna ile?

JIBU : Nilidhani angebadilika, so nilikuwa natoa nafasi. Iliposhindikana nikaona isiwe tabu, kila mtu na aubebe mzigo wake. Ukizingatia ananizidi umri miaka mingi, alitakiwa yeye anielekeze zaidi kuliko mimi kumuelekeza maisha mtu mzima.

SWALI: Uliwezaje kuondoka?

JIBU : Nilipoamua kuwa na iwe basi, Nilitoka bila kubeba kitu. Nikasafiri kwenda USA, nikakaa huko mwezi mzima ku refresh na kujipima kama kweli ntaweza ku move on? Niliporudi Tanzania sikukanyaga tena nyumbani, mpaka muda huu nnapo type na ku post haya majibu. Kwa ki fupi ni kuwa nili ondoka bila kuaga, sikuona sababu ya kuaga.

Asanteni jamani, nafikiri nimejibu yote.