Nay: Video za wasichana wakiwa wamevaa nusu ‘’Utupu’ zinauza kibiashara - MULO ENTERTAINER

Latest

7 Feb 2015

Nay: Video za wasichana wakiwa wamevaa nusu ‘’Utupu’ zinauza kibiashara



Katika hali ya kushangaza msanii wa Bongo Hip Hop,Nay Wa Mitego ametetea video ambazo hazina maadili zinazoonyesha wasichana wakiwa nusu utupu.
Picha kadhaa zimevuja kwenye mitandao ya kijamii zikumuonyesha msanii huyo akiwa kimahaba na msichana kitandani zikimaanisha kuwa kuna video yake mpya inakuja.‘’Yaah hizo picha ni za video yangu mpya ambayo itatoka hivi karibuni na kuhusu kwamba haina maadili mimi sijali na watu hajajua kama video za namna hizo zinalipa kibiashara na lazima twende na wakati mbona video za nje ambazo hazina maadili zinaonyeshwa hapa nyumbani? Alihoji Nay.

 Akizungumzia kama BASATA wakiifungia video hiyo wakati ametumia gharama kubwa alisema kuwa hajali kwa lolote ila yeye yuko tayari kwa lolote.
Video hiyo ambayo itatoka hivi karibuni inaitwa ‘only one’.