Jese and James Rodriguez kila mmoja ametupia wavuni bao moja katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Sevilla na kuifanya Real Madrid ing’ang’anie kileleni mwa La Liga kwa pointi nne safi.
Mchezaji wa Liverpool Iago Aspas anayecheza kwa mkopo Sevilla akaifungia timu yake bao la kufutia machozi ukingoni mwa mchezo.
Hata hivyo Real Madrid imepata pigo ambapo itawapoteza wachezaji wake watatu muhimu katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya wapinzani wao wa jadi Atletico Madrid.
Wachezaji hao ni James Rodriguez na Sergio Ramos walioumia huku beki Marcelo akilimwa kadi ya njano inayomfanya akose mchezo unaofuata kama Real Madrid hawatafanikiwa mpango wao wa kukata rufaa.
Rodriguez alifunga goli la kwanza dakika ya 12 na Jese akatupia wavuni bao la pili dakika 36.
Real Madrid (4-2-3-1): Casillas; Ramos (Nacho 9), Varane, Marcelo, Arbeloa; Khedira, Kroos; Bale, Rodriguez (Jese 27), Isco (Illarramendi 90); Benzema.
Sevilla (4-3-3): Beto (Rico Gonzalez 35); Figueiras, Carrico, Kolo, Navarro; Krychowiak, Iborra, Mbia; Deulofeu (Vidal Parreu - 54), Bacca (Iago Aspas 67), Vitolo