Muimbaji Maarufu nchini Rwanda Ahukumiwa Miaka 10 kwa tuhuma za kutaka Kumuua Rais Kagame. - MULO ENTERTAINER

Latest

3 Mar 2015

Muimbaji Maarufu nchini Rwanda Ahukumiwa Miaka 10 kwa tuhuma za kutaka Kumuua Rais Kagame.

A+A-
 Kizito Mihigo
Muimbaji maarufu wa Rwanda ambaye anajulikana kwa jina la Kizito Mihigo amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela baada ya kushtakiwa kwa njama za kutaka kumuua Rais Kagame na kuonyesha chuki dhidi ya serikali.
Kizito Mihigo awali alisema alikuwa na makosa na kuomba msamaha, akimaanisha hukumu yake ipunguzwe.
Mshtakiwa mwenzake, Cassien Ntamuhanga kiongozi wa kituo cha redio ya Kikristo, alifungwa miaka 25 kwa ugaidi na matusi.
Mihigo alikubali kutumiana ujumbe na kundi la upinzani lenye maskani Afrika Kusini, Rwanda National Congress (RNC).
Alifutiwa mashtaka ya ugaidi huku Ntamuhanga alifutiwa kosa la kupanga kumuua Rais Kagame