Nimemtongoza Jana, Leo Anataka Nimtumie Hela - MULO ENTERTAINER

Latest

30 Apr 2015

Nimemtongoza Jana, Leo Anataka Nimtumie Hela

Kuna msichana niliwahi kuonana nae mara1 ni rafiki wa dadaangu, tulionana nilipoenda kumtembelea sista nikahisi kumpenda, jumapili kulikuwa na event ya kifamilia nikaonana naye, safari hii nikawa siriaz kumbana nimsomeshe hadi kieleweke.

Bahati nzuri tulipotoka kwenye event tulisafiri pamoja nikakaa naye kwenye siti zinazofatana, nilimtongoza though hakunipa jibu la moja kwa moja kunikubalia but alikuwa anaonyesha kuelekea kukubali, nilimwomba namba yake akanipa. Kesho yake ambayo ni jana akanichokoza kupitia msg, akanisalimia nami nikarespond.

Si nikahisi mtoto kashakolea, ile nataka nianze kumchokoza anipe jibu langu mara akatuma meseji 'Nasikia njaa', duh ile kuendelea kuchat nikagundua anamaanisha nimtumie hela. Eti ndugu wananchi, huyu ni wife material kweli au najiingiza kwenye majanga? Maana mtu mwenyewe hela za kuokoteza.