Ali Kiba Atimuliwa Kwenye Nyumba Aliyokuwa Akiishi.......Nyumba Ilikuwa ya Mwanamke Ambaye Amechukia baada ya Kusikia Ali Kiba na Jokate ni Wapenzi - MULO ENTERTAINER

Latest

25 Jun 2015

Ali Kiba Atimuliwa Kwenye Nyumba Aliyokuwa Akiishi.......Nyumba Ilikuwa ya Mwanamke Ambaye Amechukia baada ya Kusikia Ali Kiba na Jokate ni Wapenzi



Kwa  mujibu  wa gazeti  la Risasi, pamoja na Kiba kuendelea kusisitiza kwamba si kweli, mwanamke huyo anayeishi nchini Singapore, aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kusoma kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari kuwa, kwa sasa Kiba anatoka na Miss Tanzania namba 2, 2006, Jokate Mwegelo "Kidoti" huku Kiba mwenyewe akikataa madai hayo.


"Ali (Kiba) ametimuliwa kule Kunduchi-Beach kwenye ile nyumba aliyowekwa na yule demu mwenye fedha zake na ndiye aliyekuwa akimgharamia kila kitu.

"Aliyemponza ni yule Kidoti, Jokate Mwegelo. Jokate amekuwa akimposti Kiba kwenye mitandao ya kijamii, ndipo mwanadada huyo alipoona akachukia na kumuona Kiba ameshindwa kuthamini fadhila zake," kilidai chanzo cha  gazeti  hilo.

Sasa hivi amerudi kwa mama yake, Kariakoo (Dar) kutokana na yeye mwenyewe kulikoroga kwa kuupiga teke mgodi wa fedha.

"Japokuwa mara kwa mara Kiba mwenyewe amekuwa akikanusha kujihusisha kimapenzi na Jokate, lakini ukweli ni kwamba ameshaharibu kwa mwanadada aliyekuwa anamuwezesha," kiliongeza chanzo hicho.

Katika kuweka sawa mzani wa madai hayo, mwandishi  alimtafuta staa huyo wa Ngoma ya Chekecha Cheketua kwa njia ya simu na kumuuliza kuhusu madai hayo na kutaka kujua anakoishi hivi sasa, ambapo alifunguka hivi:

"Unataka kujua naishi wapi ili iweje? Wakati unajua kabisa kuna matatizo yalinipata (kuvamiwa). Sasa nikisema si naweza kujitafutia matatizo mengine?

"Siwezi kusema ninapoishi kwa usalama wa maisha yangu na kuhusu huyo mwanamke ni maneno ya watu wenye lengo la kunichafua.

"Jokate ni mwanamke ambaye nipo naye karibu katika vitu vingine ambavyo ni vya msingi zaidi na si hivyo ambavyo watu wanahisi. Lakini kama kuna mtu atahisi tofauti itakuwa juu yake. Mimi na Jokate ni washkaji ‘long time’ (muda mrefu) katika mambo kibao.

"Kuhusu nyumba nilishawahi kufafanua kwamba siyo yangu. Kuna mtu aliniweka kwa makubaliano maalum, lakini ninashangaa kusikia taarifa ambazo zipo tofauti juu ya ukweli ambao mimi ninaufahamu."