Kauli ya Banza Stone Baada ya Kuzushiwa Kifo - MULO ENTERTAINER

Latest

25 Jun 2015

Kauli ya Banza Stone Baada ya Kuzushiwa Kifo

Baada ya kuzushiwa kifo ,muimbaji mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Banza Stone amesema si jambo la busara la kuzushiana kifo

Akizungumza kwenye AMPLIFAYA   ya  Clouds  Fm jana june 24 alisema: "Mimi nilikuwa nasumbuliwa na kichwa sana na ki homa homa fulani kama miezi miwili lakini saaa hivi niko vizuri, naelendele poa na leo nilienda hospitali daktari kufanya sound check akaniambia kuwa malaria"

Mtangazaji:…Jana ilikua ni mara ngapi kuzushiwa kifo ?

Banza Stone:.."Mimi hata sijui ila nasikia mara watu oooh banza kafa, mara ooh kila mtu anaongea lake ila mimi niko poa ni mzima naweza kufanya kazi ila kwasasa siko tayari kufanya kazi kwani nitauchosha mwili mwangu"

Mtangazaji: Vipi kuhusu kazi zako za muziki bado unaendelea nazo ama au ??

Banza Stone:….."Naweza kusema ninaendelea na muziki kama kawaida kwasababu sasa hivi nina kama nyimbo sita  mpya ziko ndani kesho, kesho kutwa naweza nikaamua niachie moja mpaka video ziko tayari sio za bendi bali ni  zangu binafsi…"