Tukio la kusikitisha sana limetokea eneo la Mbezi kwa Musuguli eneo la Bwaloni ambapo mama kwa bahati mbaya amemnywesha mwanae wa kike wa umri wa mika 3 sumu ya mende badala ya dawa ya minyoo hivyo kusababisha kifo chake. Hii ni kwasababu mama aliweka dawa ya minyoo pamoja na sumu akaamka saa 11 alfajiri ili awahi kumpa mtoto dawa ya minyoo. Kwa bahati mbaya badala ya kuchukua ile ya minyoo akachukua ile ya mende na kumpa mtoto kisha mtoto akaenda kulala.
Kulipokucha vizuri wakashangaa mtoto haamki ndipo walipoenda na kumkuta katika hali mbaya. Wakamkimbiza katika hospitali ya Bochi iliyopo Mbezi kwa Msuguli barabarani lakini walipofika waliambiwa wamechelewa sana hivyo mtoto akafariki. Amesafirishwa Jumamosi kwenda Moshi kwa mazishi. Wazazi wa mtoto ni watu waliookoka wakisali katika kanisa la KKKT Mtaa wa Bwaloni. Inasikitisha sana.
Ili kuzuia tukio kama hili kujitokeza nashauri wazazi na watu wote kuweka mbali kabisa dawa za binadamu na dawa za wanyama na wadudu iwe za kutibu au kuua wadudu. Pembeni ya hapo nimewaza sana kuwa kama tukio hili lingekuwa limefanywa na House girl kwa bahati mbaya vile vile sijui ingekuwaje?
Angeeleweka na ingeeleweka kuwa ni bahati mbaya? Katika tukio hilo mama naye alitikiswa kidogo kwani alikuwa ameilamba kidogo kabla ya kumpa mwanae.
Mungu ailaze roho ya mtoto mahali pema peponi, Ameni.