Davina : Natamani Kuchepuka Ila Nashindwa - MULO ENTERTAINER

Latest

8 Jul 2015

Davina : Natamani Kuchepuka Ila Nashindwa

Staa wa bongo movies, Halima Yahaya ‘Davina’ amekiri kuwa makundi huwa yanaharibu  watu walio kwenye ndoa kwa kuwalaghai kwamba wakaonje  nje kwa lengo  la kuangalia radha nyingine hali amabayo wakati  mwingine  mawazo hayo humjia lakini ghafla huhisi kaama mumewe atamuona na kuhatarisha ndoa yake.

Akizungimza na Tanuru la Filamu , Davina alisema  kwamba alipata wakati  mgumu wakati wakuigiza  filamu ya SHANTA inayotarajiwa kuingia sokoni  wiki hii ambayo alicheza kama mke wa mtu  ambaye  alichepiuka na mwanaume  na wakati anatoka gesti  akafumaniwa na mumewe.

“ Kweli wakati mwingine  mawazo kama haya huwa yanakuja  unaposikiliza  stori za wanawake  wachepukaji lakini huwa nafikiri nifanye hivyo kwa kukosa nini kwa mume wangu? Kutokana na msimamo huo nilipata tabu kuigiza filamu ya SHANTA ambapo  niliigiza kama  nimemsaliti mume  wangu  na kweli kwenye filamu hiyo nilifumaniwa , inakera sana wanandoa kusalitiana,” alisema staa huyo.

Davina alisema filamu hoyo itasambazwa na kampuni ya 5 Effects Movies Ltd na anaamini itawafundisha watu wengi ambao wamekuwa wakishindwa kutulia  kwenye ndoa zao ambapo  mwisho wa siku  huambulia kuambukizana magonjwa